MATATIZO KATIKA UZALISHAJI WA MBEGU ZA KIUME (LOW SPERM COUNT)

Matatizo katika uzalishaji wa mbegu za kiume inahusiana na kutokuwepo kwa mbegu za kiume kwenye manii au uwepo wa mbegu kidogo sana katika manii.
Mbegu za kiume huwa zinachunguzwa kwa kutumia kifaa maalum au darubini katika maabara, kwa kawaida mwanaume ili aweze kumpa mwanamke mimba anatakiwa atoe kiasi cha mbegu kati ya milioni ishirini hadi milioni mia tatu hamsini kwa tendo, chini ya milioni ishirini huwezi kumpa mimba mwanamke.
Endapo kiwango cha mbegu zitakuwa kidogo kitaalam hali hiyo huitwa ‘Oligospermia’ na kama huna kabisa mbegu hali hiyo huitwa ‘Azoospermia.Dalili za kutokuwa na mbegu za kiume
Hakuna dalili za moja kwa moja kusema kwamba utaumwa kitu fulani, lakini dalili zifuatazo huambatana na tatizo hili; kwanza ni kukaa katika mahusiano kwa kipindi kisichopungua  mwaka mmoja lakini mwenzi wako hapati mimba, kushindwa kufanya tendo la ndoa kwa uume kukosa nguvu’ Low sex Drive’ na  ukisimama unashindwa kuendelea na kumalizia tendo ‘Erectile dysfunction’ pamoja na kuwahi kumaliza tendo la ndoa.
Maumivu na uvimbe wa korodani, kupungua kwa vinyweleo na ndevu kutoota pia ni dalili inayoashiria matatizo ya uzazi kwa mwanaume kwani ni ishara ya upungufu wa Kromozomu au homoni za kiume.
Hizo zote ni dalili kuu za matatizo ya uzazi kwa mwanaume.
Wakati gani wa kumuona daktari?
Endapo umekaa na mwenzio mwaka mmoja au zaidi, mnafanya tendo la ndoa bila kinga yaani kizuizi chochote wakati wa kupangilia ujauzito lakini mimba haipatikani. Kama una matatizo ya nguvu za kiume au unawahi kumaliza tendo la ndoa. Unakosa hamu ya kufanya tendo la ndoa au uume unalegea wakati wa tendo pia ni mojawapo ya chanzo.
Unakuwa na maumivu ya korodani au korodani kuvimba, maumivu ya uume na maumivu wakati wa kukojoa au uwepo wa kivimbe katika uume.
Chanzo cha tatizo
Uzalishaji wa mbegu za kiume unafuatana na ubora wa korodani kama haina tatizo lolote na kiwango bora cha mfumo wa homoni mwilini mwake. Homoni zinadhibitiwa katika ubongo na kuimarisha korodani zizalishe mbegu. Mbegu zikishazalishwa, husafirishwa na mirija midogo sana na laini hadi katika tezi dume’Prostate gland’ ambayo kazi yake kubwa ni kuzalisha manii.
Matatizo katika mbengu za kiume ni kutokuwepo kwa mbengu kunakosababishwa na hitilafu kwenye korodani, kuzalisha mbegu zenye kasoro, mbegu zisizo na kiasi na mbegu chache.
Matatizo ya korodani husababishwa na joto kali katika korodani, maambukizi katika korodani na uume na kuumia korodani.
Mishipa ya damu kulalia korodani ‘Variocele’ pia ni mojawapo ya tatizo kubwa la kuziba kwa mirija ya usafirishaji mbegu hizo.
Zipo pia sababu za kimazingira zinazoathiri uzalishaji wa mbegu za kiume mfano kemikali za viwandani, rangi za viwandani au majumbani, dawa za mashambani na za kuua wadudu, mionzi  ya X- Ray, kukaa kwenye joto kali, kuvaa nguo za kubana na kukaa mahali kwa muda mrefu, kupakata kompyuta  ‘Lap top’ kwa muda mrefu, matumizi ya sigara, bangi na madawa mengine ya kulevya kwa muda mrefu na ulevi uliokithiri. Uzito mkubwa wa mwili na matatizo ya akili.
Uchunguzi
Uchunguzi wa tatizo hili  hufanyika katika hospitali za mikoa na wilaya kwa madaktari wa masuala ya uzazi.
Vipimo vya damu kuangalia mwenendo wa mfumo wa homoni mwilini Kipimo cha Ultrasound kuangalia korodani yako kwa ndani.
Uchunguzi hufanyika kisayansi hospitali tu, hakuna vifaa vingine vya kuchunguza kwa kubahatisha, unatakiwa utolewe damu, na utoe mbengu zako za kiume baada ya kupumzika kufanya tendo la ndoa  angalau kwa siku tatu.
Matibabu na ushauri
Hufanyika baada ya uchunguzi ambapo daktari atatoa dawa kuzingatia na tatizo lililopo.
Kama hakuna mbegu  zipo chache au kuna maumivu au kasoro zozote.Uwepo wa kasoro za viungo vya uzazi pia ni tatizo mfano, uume mfupi, kutokuwa na korodani au kuwa na korodani moja. Wahi hospitali kwa uchunguzi na tiba.
Salut kwa GPL
TUPE MAONI YAKO

Siku Rais Museveni Aliponusurika Kutekwa Nairobi..Stori kamili hii hapa


YKM2
Ndugu zangu,
Kuna matukio makubwa yalitokea sambamba na Vita Vya Kagera vilivyokuwa vikiendelea mwaka 1978. Kwenye kitabu chake ' Sowing The Mustard Seed', Yoweri Museveni anasimulia tukio la kijasusi mlengwa akiwa ni yeye.
Museveni alikuwa Nairobi kukutana na baadhi ya Waganda wanaharakati. Ndani ya intelijensia ya Tanzania, kulikuwa na mkakati wa kushawishi uasi wa kijeshi ndani ya jeshi la Idi Amin. Museveni alishirikishwa.
Pale Nairobi, Museveni alikuwa akitembea akigawa kwa Waganda wanaharakati nyaraka zenye hotuba ya Julius Nyerere.
Makachero wa Kenya walizinasa harakati za Yoweri. Wakapanga kumnasa Museveni. Walimtuma jasusi Mzungu mwenye uraia wa Kenya. Aliitwa Patrick Shaw. Huyu alikuwa jasusi lilokubuhu na inasemwa alikuwepo kwenye mpango uliotekelezwa wa kumteka na kumwua mwanasiasa wa Kenya wa enzi hizo, J. M Kariuki, mwaka 1976.(P.T)
Museveni anasimulia, kuwa alipokaa na rafiki yake akinywa kahawa mgahawani, Nairobi Hilton Hotel, ghafla, alimwona mzungu mnene mwenye madevu akiingia. Alikuwa jasusi Patrick Shaw.
Jasusi Shaw alikaa mbali kidogo na Museveni. Akachukua gazeti na kujifanya analisoma huku akitupa jicho kwa kuvizia kwa Yoweri Museveni.
Museveni akafanya maamuzi ya haraka, akamwambia rafiki yake abaki hapo hapo. Naye Museveni akakunjua gazeti kujifanya yuko bize analisoma. Kisha akaagiza kahawa nyingine. Muhudumu alipokuja nayo tu, basi, Museveni, akainuka kujifanya anakwenda haja ndogo. Ikawa kimoja...breki ya kwanza ikawa Namanga.
Nini kilimtokea Museveni alipofika Namanga, bila passsport wala nyaraka nyingine za kumwezesha kuvuka mpaka kuingia Tanzania?
Kesho nitasimulia, panapo majaliwa...
Maggid,
Iringa.
Chanzo;www.mjengwablog.com
TUPE MAONI YAKO

Dk Mwakyembe: Hatutazuia magari ya kitalii toka nchi jirani


 
Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dk Harrison Mwakyembe (katikati) akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, kushoto ni Katibu mkuu wa Wizara hiyo Joyce Mapunjo na kulia ni Naibu waziri wa Wizara hiyo  Dr. Juma Abdulla Saadala. Picha na Emanuel Herman  

 Waziri Ushirikiano wa Afrika Mashariki  Dk Harison Mwakyembe amesema Tanzania haitazuia magari ya . Nchi Wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki au Nchi nyingine kuingia katika viwanja vyake vya ndege kuleta au kuchukua Watalii wanaopitia katika viwanja hivyo na kwenda katika nchi zao.
Akizungumza na waandishi wa hahabari jijini Dar es Salaam jana, Dk. Mwakyembe  amesema serikali ya Kenya wameenda kinyume na mkataba wa mwaka 1985 kwa kuvihusisha viwanja vya ndege kuwa sehemu ya vivutio vya utalii jambo lililopelekea kukatazwa kwa magari ya Kitalii yaliyo sajiliwa Tanzania kuingia uwanja wa ndege wa Jomo Kenyata.

Dk Mwakyembe amesema  Waziri wa Maliasili na Utalii tayari ameshafanya mazungumzo na Waziri wa Maliasili na Utalii Kenya katikati ya mwezi Januari  ,2015 lengo la kikao hicho ilikuwa ni kutafuta ufumbuzi wa kudumu wa kukatazwa kwa maghari katika uwanja wa ndege wa Kenya

 “Suala la kurekebisha mkataba ulioingizwa na nchi hizi mbili kwa hiari miaka 30 iliyopita si jepesi, linahitaja mjadala mrefu utakaohusisha taasisi mbalimbali. Hata hivyo vyombo husika vinafanyia kazi suala hilo,amesema Dk Mwakyembe

Amesema Tanzania itachukua hatua ya kuwafahamisha Watalii na wageni wote wenye nia ya kutembelea vivutio vya kitalii vya Tanzania kutumia viwanja vingine vya ndege ili kuepusha kadhia na gharama zisizo za lazima.

Dk Mwakyembe aliongeza kuwa  suala la Magari ya Tanzania kukatazwa kuingia kwenye kiwanja cha Jomo Kenyatta nchini Kenya halitakiwi kabisa kurudisha mahusiano mema miongoni mwa nchi hizi mbili.
Tembelea www.meac.go.tz kupata habari mbalibali zihusuzo nafasi ya Tanzania katika Jumuiya ya Afrika Mashariki..
Salut kwa Gazeti la Mwananchi
TUPE MAONI YAKO
 

SULEIMAN MAGOMA Copyright © 2011 -- Template created by Suleiman Magoma -- Powered by Magoma Co.LTD