STAR WA BONGO MOVIE ALI YAKUTI ANASURIKA NA AJALI MBAYA.

Ali Yakuti


Ali Yakuti Mwandishi wa muswada ya filamu mahiri aliyepata ajali .
MWANDISHI wa muswada mahiri katika tasnia ya filamu Swahiliwood Ali Yakuti mwisho mwa wiki alipaja ajali mbaya katika maeneo ya Mbezi kibanda cha Mkaa, na kumsababishia maumivu makali, mwandishi huyo alikutwa na dhahama hiyo wakati akijiandaa kuvuka barabara ambapo gari yenye namba za usajili T530 EAS lilimfuta na kumgonga pembeni.

Ali Yakuti
Ali Yakuti akiwa katika moja ya filamu alizowahi kuigiza.
ramsey noah ,sammy shoo, ali yakuti
Ali Yakuti akiwa na Steven Shoo na mwigizaji wa kimataifa kutoka nchini Naijeria Ramsey Noah.
Ali Yakuti
Ali Yakuti akiwa kazini.
Ajali hiyo ilimsababishia maumivu na kuchukuliwa na wananchi waliokuwa maeneo hayo na kukimbizwa katika Hospitali ya Tumbi Kibaha alipatiwa matibabu kutokana na majeraha aliyokuwa nayo sehemu ya kichwa na mkono wa kushoto, sehemu ya kichwa alishonwa nyuzi 8 huku mkono akishonwa nyuzi sita.
“Nashukru Mwenyezimungu baada ya matibabu ninaendelea vizuri hata maumivu yamepungua kwa kiasi fulani, ilikuwa ajali mbaya unajua ukiwa kando ya barabara hautegemei kufuatwa na gari kwani ini sehemu ambayo inaonekana salama,”anasema Ali Yakuti.
Yakuti amewashukru wadau wote ambao walipopata taarifa walimpigia simu na kumtumia ujumbe kwa ajili ya kumpa pole, anasema kuwa anawashukru sana Mungu awabariki wote kwani si rahisi kwa kila mtu kumtaja kwa jina, kwa sasa anaendelea vizuri na afya yake imetengemaa.
Kopata more stories za bongo movie tembelea hapa
TUPE MAONI YAKO

Huyu ndiye mdogo wa KANUMBA aliye ahidi kubeba mikoba ya kaka yake


Seth Bosco
Seth Bosco mwigizaji wa filamu Swahiliwood.
MSANII Seth Bosco ambaye ni mdogo wake na msanii nyota aliyetikisa tasnia ya filamu nchini marehemu Steven Kanumba amekusudi kufunika pengo liloachwa na marehemu kaka yake akiongea na Mwanaspoti msanii huyo amesema katika kumuenzi kaka yake ni kuhakikisha kuwa kampuni inaendelea na kufanya kazi za filamu zenye nzuri na ubora.

Seth Bosco
Seth Bosco akiongea na vyombo vya Habari havipo pichani.
Filamu ya Malaika
Filamu ya Malaika filamu ya kwanza akiwa kinara
“Baada ya kumaliza msiba na taratibu zingine kampuni ya Kanumba Great Film inaendelea na kazi zake kama awali na kufanya katika ufanisi wa hali ya juu, nakumbuka hosia wake juu yangu na kwa kufuata hayo namuenzi kwa kutengeneza filamu ya Malaika ambayo mimi ni mhusika,”anasema Seth.
Seth licha ya kuwa ni mdogo wake na marehemu lakini pia ndio aliyekuwa mtu wa karibu na marehemu Kanumba, katika filamu hiyo ya Malaika Seth anaigiza na mwanadada Rose Ndauka ambaye pia aliwahi kufanya kazi na marehemu, wasanii wengine wanaoshiriki katika filamu hiyo ni Abdalah Mkumbila ‘Muhogo Mchungu’, Maya na wengine wengi.

TUPE MAONI YAKO

EXCLUSSIVE PICTURES ZA FLAVIAN MATATA ALIPOTEMBELEA BBC KWA AJILI YA INTERVIEW


 The supermodel and former Miss Universe Tanzania (2007), Flaviana Matata, was in the UK for the London Fashion Week.
She spoke to the BBC a few hours before returning to New York where she is based when not working in Europe, Africa or other parts of the world. Here she is being interviewed for BBC Africa’s news and current affairs TV programme in Kiswahili, Dira ya Dunia.
 She was also interviewed for BBC's Focus on Africa radio programme. Listen to the interview at 1500 GMT. It will also appear on our podcast.
 Flaviana posing with BBC Africa's very fashionable presenter Kassim Kayira
 Flaviana with Jestina George of www.jestina-george.com (a blogger based in London) at the BBC studios in London
For the interview Flaviana rocked  a leather jacket from Zara, Dress from Mango, Gucci sunglasses & gorgeous shoes from McQueen.
******
Tanzania's supermodel Flaviana Matata has had a very busy schedule and to be precise she's been busy on the runway between New York  & London. 

At the moment Flaviana is in the UK where she has just taken part in London Fashion Week.
Earlier today Flaviana visited the BBC  Africa studios in London where she was interviewed for BBC Africa’s news and current affairs TV programme in Kiswahili, Dira ya Dunia  &  for Focus on Africa.

The former winner of Tanzania's first Miss Universe pageant, in 2007, started by telling how she got into the fashion industry and later dished out on the latest tips on what is fashionable these days.


Below is the link where you can listen to the Focus on Africa interview. It is also being currently promoted on the BBC’s Entertainment & Arts pages. 
 For more African news from the BBC download the Africa Today podcast.

 Photo credit: Manuel Toledo, BBC Africa
TUPE MAONI YAKO

KOCHA WA YANGA AZUA JAMBO HUKO MBEYA NA KUPELEKEA TIMU HIYO KUSHTAKIWA

TAARIFA YA UONGOZI WA HOTEL YA PETER SAFARI’s KWA VYOMBO VYA HABARI KUHUSIANA NA MADAI YALIYOTOLEWA NA KOCHA WA TIMU YA YANGA BAADA YA KUMALIZIKA MCHEZO WAKE NA TANZANIA PRISON TAREHE SEPT 15, 2012.
Ndugu wanahabari,
Karibuni katika mkutano mfupi ambao unalenga kuzungumzia  ama kuelezea masikitiko makubwa dhidi ya Kocha wa Timu ya Yanga TOM SAINTFIET aliyoyatoa kwa vyombo vya habari kuidhalilisha hoteli  yangu   juu ya huduma zake na kiwango chake alichokiita cha huduma 
mbovu!.
Kimsingi management ya  Peter safari’s Hotel na Uongozi wa chama cha wamiliki wa Mahotel Mkoa wa Mbeya, tumesoma na kusikiliza kwa masikitiko makubwa lawama zilizotolewa na Kocha huyo kuwa “hajawahi kulala kwenye hoteli ya hadhi ya chini kama hii  katika nchi 20 alizowahi kufanya kazi katika nchi za Afrika”.
Uongozi wa hotel  na chama cha wamiliki wa hotel kwa ujumla kinachukulia suala hili kama kampeni maalumu ya kudhalilisha na kukatisha tamaa wateja kuiona mbeya haina hotel za hadhi za kuishi timu na watu wenye hadhi katika jamii, kitu ambacho si kweli na ni visingizio kutokana kushindwa kwake kuwezesha timu kufikia matarajio  ya mashabiki na wapenzi wa timu hiyo.
Kimsingi viongozi wa Timu ya Yanga waliomba kuwalaza wachezaji wawili katika kitanda kimoja tofauti na taratibu za hotel na hii ilitokana na mipangilio yao hasa kwenye suala la uwezo wa kulipia kila mchezaji chumba chake, aidha, uongozi wa hotel ulijitahidi kwa kadri ya uwezo wake kuhakikisha kuwa wachezaji wanapata huduma walizohitaji na hata wakati mwingine kutoa usafiri kwaajili ya kununua mahitaji ya familia zao kitu ambacho hakifanyiki maeneo mengine kwa gharama za hotel.
Kwa kutambua madhara yaliyotokana na matamshi ya kocha huyo raia wa Ubelgiji, Uongozi wa hotel ya Peter Safaris  unayaona matamshi haya kama udhalilishaji mkubwa  na wenye nia mbaya ya kuuharibia mkoa wa Mbeya  na kuutangaza vibaya kwa wageni  juu ya uwezo wake katika utoaji wa  huduma za hoteli.
Aidha  kwakuwa maneno ya kocha huyo  yametamkwa na kutangazwa kwenye vyombo vya habari pasipo kukanushwa na viongozi wa Timu ya Yanga ambao ndiyo waliofanya maandalizi na kufanya mazungumzo ya maombi  ya kuwalaza wachezaji wawili katika vyumba ambavyo vina uwezo wa kulaza mtu mmoja (single), Peter safaris inaliona jambo hilo kama ni sehemu ya kashfa iliyojengwa kwa nia ya kuiharibia hotel biashara  na kuipotezea hadhi mbele ya wageni  na watumiaji wa huduma za PETER SAFARIS  ambayo inaendelea kupanua huduma zake kwa mkoa wa Mbeya na maeneo mengine.
Ikumbukwe kuwa Peter safaris hotels imekuwa ikipokea wageni wa hadhi mbalimbali wakiwemo viongozi wa ngazi za kitaifa, wageni kutoka nje wa hadhi za juu na wafanyabiashara wakubwa, hivyo ugeni wa Yanga na hadhi inayozungumzwa na Kocha huyo hauwezi kufikia mahala pa kuidhalilisha hotel kwa kiwango hicho ambacho kocha huyo amevitumia vyombo vya habari licha ya hotel kutopata maoni yoyote baada ya timu  kuhudumiwa   kwenye sanduku la maoni(suggestion box).
Kutokana na hali hii iliyojitokeza, uongozi wa Hotel unautaka uongozi wa Yanga kuiomba radhi management ya Hotel ya Peter safaris kwa lugha ya kashfa na isiyoendana na utamaduni wa Mtanzania kwakuzingatia kuwa wachezaji wakiulizwa namna walivyohudumiwa wasingeweza kuzungumza hayo ambayo mwalimu wao ameyazungumza kwa utashi wake.
PETER SAFAR’s inalichukulia jambo hili kwa uzito unaostahili kwakuzingatia kuwa  lugha iliyotolewa na mteja wake huyo imevuka kiwango cha kuvumilika, na njia pekee ambayo tunadhani ni ya uungwana kabla ya kuingia kwenye taratibu za kisheria ni kuwataka YANGA kuomba radhi kwa lugha ya dharau na kashfa dhidi ya hotel yetu vinginevyo tunakusudia kuchua hatua za kisheria kwa kuzingatia kuwa hotel inaendeleshwa kwa mujibu wa taratibu na sheria zinazotawala huduma za hotel na zile za mipango miji
 ambazo masuala ya usafi ni miongoni mwa maeneo muhimu ya kukidhi viwango vya uendeshaji wake.
Ninawashukuruni kwa  mahudhulio yenu
Nawasilisha
MKURUGENZI  MTENDAJI
PETER SAFARI’s HOTEL MBEYA.  
20/09/2012
TUPE MAONI YAKO

KAMA UMEMIS KUANGALIA HARD NEWS ZA KIMATAIFA ZA AL JAZEERA NDIO MUDA WAKO SASA


TUPE MAONI YAKO

Taharuki kuhusu filamu ya Marekani

Maandamano Pakistan
Ulinzi umedhbitia katika nchi nyingi za kiisilamu huku zikijiandaa kwa maandamano makubwa hii leo baada ya maombi ya Ijumaa.
Maandamano hayo yanapinga filamu iliyotengezwa nchini Marekani kumkejeli Mtume Muhammad na dini ya kiisilamu.
Nchini Pakistan, serikali imetenga siku maalum kwa jina "special day of love" kwa miniajili ya kumsifu Mtume Muhammad.
Marekani imelipia matangazo ya kibiashara nchini Pakistan, rais Obama akionekana kukashifu vikali filamu hiyo
Maandamano makubwa kupinga filamu hiyo tayari yamesababisha vifo sehemu mbali mbali duniani.
Ingawa Marekani ndiyo imeathirika zaidi kutokana na mandamano hayo, uchochezi umeoneka kuongezeka kutoka barani Ulaya baada ya jarida moja nchini Ufaransa kuchapisha picha za kumfanyia mzaha Mtume na waisilamu waliopinga vikali filamu hiyo.
Pakistan imetoa wito kwa watu nchini humo kuandamana kwa amani.
Vyama vyote rasmi vya kisiasa pamoja na mashirika ya kidini wametangaza maandmano kwa ushirikiano na makundi ya kibiashara huku maandamano hayo yakitarajiwa kuwa makubwa sana.
Waziri wa mambo ya nje nchini humo, Hina Rabbani Khar, ameambia shirika la habari la AP kwamba siku hiyo maalum inanuiwa kushinikiza maandamano ya amani na kuzuia watu wenye msimamo mkali kusababisha ghasia kutokana na hasira yao dhidi ya Marekani.
Duru zinasema kuwa vituo vya mafuta, maduka na masoko yatafungwa leo na huenda usafiri ukasitishwa .
CHANZO; BBC
TUPE MAONI YAKO

NOMA; GERARD PIQUE AMJIBU MESSI - AMJAZA MIMBA SHAKIRA

Hips hazidanganyi na vipimo vya mimba pia: Shakira ni mjamzito!

Mwanamuziki huyo wa kilatini, 35, alitumia ukurasa wake wa Facebook kutangaza kwamba anatarajiwa kupata mtoto wake wa kwanza na mwanasoka wa kimataifa wa Hispania na klabu ya Barcelona Gerard Pique, aliandika, "Kama baadhi yenuu mnavyojua, Gerard na mimi tuna furaha kwa kutarajia kupata mtoto wetu wa kwanza!"

"Tumeamua kuupa umuhimu wakati hu mzuri sana kwetu katika maisha yetu na kuhairisha kila kitu kuhusu kazi zangu nilizozipanga kufanya hivi karibuni," alisema Shakira na kuongeza. "Hii inamaanisha sitokuwepo katika tamasha la iHeartRadio."

Kwa taarifa hiyo Gerard Pique anaungana na Lionel Messi ambaye nae anasubiri nae kuitwa baba miezi kadhaa ijayo .
chanzo; shafiidauda.com
TUPE MAONI YAKO

HII NDIO TOFAUTI YA KATI YA MABASI YA SIMBA NA YANGA NA LA GOR MAHIA YA KENYA

 yasemekana hili ni basi lililo nunuliwa na mashabiki wa Gor Mahia kwa ajili ya timu yao
 
 
 Mabasi ya Simba na yanga - PICHA KWA HISANI YA http://moronew.blogspot.com
TUPE MAONI YAKO

HIKI NDICHO ALICHOKISEMA KOCHA WA YANGA BAADA YA TIMU YAKE KUPOKEA KICHAPO CHA 3-0


Akizungumza baada ya mazoezi ya timu hiyo yaliyofanyika Uwanja wa Kaunda Dar es Salaam asubuhi jana, Saintfiet alisema Yanga ingeweza kuibuka na ushindi kama washambuliaji wake wangetumia vizuri nafasi nane walizopata kwenye mechi hiyo.
“Sisemi kama wangetumia nafasi zote walizopata, lakini wangetumia baadhi ya hizo tungeweza kushinda mechi hiyo, pia tulipata penalti ambayo tulikosa,”alisema Saintfiet.
Washambuliaji wa Yanga juzi walikuwa ni Hamisi Kiiza na Said Bahanunzi, ambapo Kiiza pia alipoteza penalti.
Alikanusha kupenda kutumia mfumo wa kujihami ambao wachambuzi wa soka wanasema ndio chanzo cha kuinyima timu hiyo ushindi kwenye mechi zake, kwa kusema alicheza na washambuliaji wawili kwenye mchezo huo na ndio maana waliweza kutengeneza nafasi nyingi za kufunga.
Saintfiet alisema pia safu yake ya ulinzi ilijichanganya kwenye mechi hiyo kiasi cha kuruhusu mabao mawili ya kwanza na kusema bao la tatu la Mtibwa lilifungwa kwa mkwaju wa mbali na hivyo anaona kama lilitokana na ubovu wa mabeki wake kutojipanga sawasawa.
“Tuna mabeki bora Afrika lakini mabao mawili ya kwanza yalitokana na kujichanganya kwao, bao la tatu lilifungwa kwa shuti la mbali,”alisema Saintfiet.
Pia aliendelea kuilalamikia ratiba ya Ligi Kuu kwani inaipendelea sana Simba kwa kucheza mechi tatu zote nyumbani na wao kucheza mechi mbili ugenini, ingawa alisema wanajipanga kwa ajili ya mchezo dhidi ya JKT Ruvu ambao amesema utakuwa mgumu lakini wamejiandaa kushinda kujiweka kwenye msimamo mzuri kwenye ligi.
Kocha huyo alisifu mazingira ya hoteli waliyofikia mjini Morogoro kuwa ilikuwa na huduma nzuri za maji, chakula na kila mchezaji alilala kwenye chumba chake tofauti na hoteli waliyofikia Mbeya ambapo alidai wachezaji walilazimika kulala wawili kwenye kitanda kimoja.
Timu hiyo ilirejea Dar es Salaam jana asubuhi ikitokea Morogoro na moja kwa moja wachezaji walienda mazoezini.
Wakati huohuo, Kocha Mkuu wa Simba, Milovan Cirkovic amelalamikia kadi nyekundu aliyeoneshwa mshambuliaji wa timu hiyo, Emmanuel Okwi kwenye mechi dhidi ya JKT Ruvu juzi, ambayo Simba ilishinda mabao 2-0.
Akizungumza baada ya mechi hiyo, Milovan alisema mshambuliaji huyo wa kimataifa wa Uganda alis tahili kuoneshwa kadi ya njano kutokana na kosa hilo na siyo kadi nyekundu.
“Nimefurahi kupata pointi tatu muhimu, mchezo ulikuwa mgumu lakini wachezaji wangu walicheza vizuri na kupata matokeo,”alisema Milovan.
Okwi mshambuliaji tegemeo wa timu hiyo alioneshwa kadi nyekundu kwa kumpiga kiwiko beki wa JKT Ruvu, Kessy Mapande akiwa hana mpira baada ya muamuzi Andrew Shamba kuamuru faulo ipigwe kuelekea lango la JKT Ruvu na ndipo Okwi alimfuata mchezaji huyo na kumpiga kiwiko hali inayomuweka kwenye wakati mgumu wa kufungiwa mechi tatu kutokana na kanuni za ligi hiyo.
Kwa upande wake kocha wa JKT Ruvu Charles Kilinda alisema kadi aliyooneshwa mshambuliaji huyo ilikuwa halali kwani ni dhahiri alimpiga kiwiko beki wa timu yake.
Kuhusu mchezo Kilinda alisema timu yake iliruhusu mabao ya kizembe na kusema sasa wanajipanga na mchezo dhidi ya Yanga Jumamosi.


Tom Saintfiet
KIPIGO cha mabao 3-0 ilichokipata Yanga juzi kutoka kwa Mtibwa Sugar Uwanja wa Jamhuri Morogoro bado kinamtesa Kocha Mkuu wa timu hiyo, Tom Saintfiet huku akiwalaumu washambuliaji wake kwa kutokuwa makini.
MSIMAMO LIGI KUU BARA
Na   Timu                      P  W  D  L  GD  Pnt
1    Simba SC                2   2   0  0   5    6
2    Mtibwa Sugar          2   1   1   0   3   4
3    Azam FC                 2   1   1   0   1   4
4    Coastal Union          2   1   1   0   1   4
5    Shooting                 2   1   0   1   0   3
6    JKT Ruvu                 2   1   0   1  -1   3
7    African Lyon            2   1   0   1  -2    3
8    Toto Africa              2   0   2   0   0    2
9    Prisons FC               2   0   2   0   0    2
10  JKT Oljoro               2    0   2   0   0    2
11  Kagera Sugar          2    0   1   1  -1    1
12  Polisi                      2    0   1   1  -1    1
13  Yanga                     2   0    1   1  -3    1
14  Mgambo                 2   0    0   2   -2   0
CHANZO; MILLIONFORTUNE
TUPE MAONI YAKO

HII NDIO FURAHA YA KUMALIZA SHULE, WAHITIMU DARASA LA SABA WALONGA


Wanafunzi wa Shule ya Msingi ya Mnazi Mmoja, Dar es Salaam wakifurahia na sahani zao za chakula baada ya kumaliza mtihani wa kuhitimu darasa la saba shuleni hapo jana. (Picha na Fadhili Akida).
 
KILA MMOJA KIONYESHA FURAHA KWA KUMALIZA SALAMA ELIMU YA MSINGI

HONGERENI SANA WANAFUNZI WOTE MLIOMALIZA DARASA LA SABA!
Kupata ma stori mengine motomoto tembelea hapa
TUPE MAONI YAKO

HUYU NDIYE MSHITAKIWA ALIYETAPELI KAMPUNI KWA KUTUMIA JINA LA DR. ASHA ROSE MIGIROMshitakiwa katika kesi ya utapeli dhidi ya Kampuni ya wakala wa kupakia na kupakua mizigo bandarini ya Mokha Agency Co. Ltd ya Dar es Salaam, aliyedaiwa kutumia jina la aliyekuwa Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa (UN), Dk Asha-Rose Migiro, Sharifa Kalala (nyuma) akiongozwa na askari wa Mahakama ya Wilaya ya Ilala, Dar es Salaam kwenda kupanda karandinga baada ya kusomewa mashitaka mahakamani hapo jana.
TUPE MAONI YAKO

EXCLUSSIVE PICTURES ZA NYUMBA ANAYOISHI NA ANAYOMILIKI MSANII TUNDA MAN WA TIPTOP CONNECTION

Nyumba iko Mabibo Dar es salaam na inamilikiwa na Tunda Man msanii wa bongofleva kutoka Tiptop Connection.
.
Hiyo sehemu yenye kioo ni maalum kwa ajili ya dancers wake kufanya mazoezi.
.
.
.
.
.
.
.
Mtoto pekee wa Tunda Man.
Hapa ndipo anapolala Tunda Man.
.
.
.
.
.
.
.
TUPE MAONI YAKO

HII NDIYO PICHA YA SIKU


 
Afande sele na wema sepetu
TUPE MAONI YAKO

KUMBE HATA MTONI KUNA MASTAR WASHAMBA, DMX amesema hajui kutumia computer kabisa, eti inamuogopesha hata kuiangalia!

Rapper mwenye sauti ya kipekee hasa kwenye miondoko ya Hip Hop DMX, ameweka wazi kuwa ameshindwa kabisa kuendana na ukuaji wa sayansi na teknolojia kwa sababu hawezi kabisa kutumia computer, iwe desktop ama laptop.

DMX ambae ni member wa zamani wa kundi la Ruff Ryder amesisitiza kuwa  hana uwezo kabisa wa kutumia laptop wala desktop computer, kitu ambacho kwa ulimwengu huu sio cha kawaida hasa kwa mtu kama yeye mwenye jina kubwa na ambae habari zake nyingi zinazomhusu zinatokea sana kwenye mitandao mbali mbali.

Sio kwamba hana uwezo wa kujifunza zaidi kwa sababu elimu haina mwisho, lakini yeye hataki hata kujifunza kuhusu matumizi ya computer, na kila anapoiangalia computer anaona kama ina vitu vya kuogofya. Katika interview aliyofanya na Power 105.1 X alisema “angalia vitu vyote hivi, it’s scary, ina mambo mengi mno, naapa kwa jina la bibi yangu kweli tena hadi nashindwa kuwa mvumilivu kiasi hiki..Errr!ningeweza hata kuivunja” alisema DMX.

Hakuishia hapo akaongezea kuwa yeye kwake Google hata haina maana kabisaaa, na haimuingii akilini ni kama kichekesho flani, “it’s funny, it’s weird”.
Alipoulizwa yeye akitaka kuchek habari zinazomhusu yeye mwenyewe inakuaje kama anaogopa computer na hajui kuitumia, alisema yeye huwa anatumia simu yake na ndiyo anaielewa na sio laptop na desktop computer, “I know how to do it on a phone”.

DMX anaweza kuwa sio rappa pekee ambae ametamka hadharani kuwa hana ukaribu sana na hii teknolojia inayokuwa, wapo wengi ambao hata mambo ya tweeter kwao wanaona hayana maana, kama utakumbuka pia hasimu wa DMX kwa sasa na rapper wa Young Money Drake, aliwahi kukiri kuwa hakuwa na urafiki na internet enzi hizo bado anatafuta jinsi ya kutoka akiwa anafanya mixtape tu, hata nyimbo za 50 Cent na Kanye West alikuwa na CD zao na sio soft copies, lakini yeye alikiri jinsi internet ilivyomsaidia sana, ambapo nyimbo zilizokuwa kwenye Mixtape yake zilipoingia tu kwenye internet sauti yake ikakita kwenye sikio la boss wake wa Young Money Lil Wayne na kwa jinsi alivyomteka attention Lil Wayne akamsaka na kum-sign Young Money.
Haya kama hawa wa huko duniani ambao ndio huwa tunawaangalia na kufuata nyayo zao kwa kuamini wao wameendelea wanafeli hivi, je kuna usalama kweli kwa wasanii wa kibongo ambao baadhi yao hua wanaiga tu vitu bila kujali kama havina manufaa ilimradi kachukua kutoka kwa msanii wa marekani? Huu sasa ni wakati wa wasanii wetu wa Tanzania kuelimika na kuiga yale tu ya maana na yanayoweza kuwaletea maendeleo na kuachana na mambo mfano kama huu wa DMX.
TUPE MAONI YAKO

AUNTY LULU ATIMULIWA NA MWENYE NYUMBA

Lulu Mathias Semagongo 'Aunty Lulu'.
Na Gladness Mallya
MWANADADA asiyeishiwa na matukio Bongo, Lulu Mathias Semagongo 'Aunty Lulu' amefukuzwa kwenye nyumba aliyokuwa anaishi Kinondoni jijini Dar es Salaam kutokana na mmoja wa wanaume aliokuwa akiishi nao anayedaiwa kuwa 'si riziki' kufumaniwa akifanuya uchafu chooni.
Akizungumza na Ijumaa, mmoja wa majirani wa Aunty Lulu ambaye hakutaka jina lake lichorwe gazetini alisema mwanadada huyo pamoja na wanaume aliokuwa akiishi nao walifukuzwa wiki iliyopita na mwenye nyumba baada ya kubaini kuwa, wanatumia chumba chao kufanya ufuska.
“Yaani sijui kwa nini Aunty Lulu alikuwa anawang’ang’ania wale mashoga, yaani walikuwa wanatusumbua kweli mpaka mwenye nyumba kaamua kuwafukuza, kitendo cha kufumwa chooni siyo cha mara ya kwanza, hii ni mara ya pili,” alisema jirani huyo.
Baada ya kuzinyaka ‘nyuuzi’ hizo paparazi wetu alimtafuta Aunty Lulu ambapo alikiri kufukuzwa ndani ya nyumba hiyo kutokana na tabia za wanaume hao ambao walikuwa wamepinda ile mbaya.
“Ni kweli, wale watoto wameniharibia sana na sasa naishi kwetu huko Mbezi wakati natafuta chumba kingine,” alisema Aunty Lulu.

CHANZO; GLOBAL PUBLISHERS
TUPE MAONI YAKO

HIKI NDICHO ALICHOKISEMA RAPPER NAY WA MIITEGO KUHUSU BONGO MOVIE STAR JB

Msanii wa muziki  hapa  nchini, Ney wa Mitego jana amemuangushia bomu muigizaji wa filamu nchini, Jacob Steven aka JB kuwa hana tofauti na waigizaji wa Bongo Movies anaowachukulia kama vicheche.

Kauli hiyo ameitoa jana kwenye kipindi cha Hot Mix cha EATV baada ya hivi karibuni kukwaruzana na JB jijini Mwanza kwenye ziara ya Fiesta. Inadaiwa kuwa Ney alimwita Wema kicheche jukwaani jambo lililomfanya muigizaji huyo kukwaruzana na Ney.

“JB alikuwa kama mtoto mdogo au ulifika time wacha tu niliongee hili,” alisema Ney.

 Ilifika time nikasema JB simtofautishi na wale akina Aunty Ezekiel sijui akina Wema kwasababu unajua mtoto wa kike ni dhaifu unajua, mimi nilimsamehe Aunt Ezekiel na Wema pia, sababu Wema na Aunty Ezekiel ni watu waliotaka kugombana na mimi, niliwasamehe palepale.

 Nachokisema sio kama nabahatisha, nakuwa na uhakika nacho. JB na Ray ilibidi waungane pamoja wanifuate, ‘bwana unajua mimi ni dogo kwao’ lakini labda tunashindana tu vitu fulani, ukubwa wa umri si tatizo.”

Uhusiano mbaya kati ya waigizaji wa filamu nchini na Ney ulianza baada ya rapper huyo kudai kwenye wimbo wake‘Nasema Nao’ kuwa makahaba wenye kiwango wapo kwenye Bongo movies.
TUPE MAONI YAKO

PRODUCER C9 MBIONI KUVUTA JIKO NA TAYARI KASHATOA POSA

WAKATI vijana wengi wa mjini wakiwa na kasumba ya kutoweza kuishi na mwanamke hasa yule anayetokea kijijini, producer anayeshika kasi town kutoka studio ya Kiri Records, C9, amedai kuwa kwa upande wake haoni kama kuna tatizo kwani tayari ameshatoa mahari kijini kwao kwa ajili kuoa ingawa mmwamke huyo alishawahi kuishi mjini miaka kadhaa.

C9 alidai kuwa alisafiri na kwenda nyumbani kwa mama yake Songea vijini na hatua ya kwanza aliyoifanya ni kumpa mama yake taarifa hiyo ya kutaka kuoa ingawa wengi hawakuamini baada ya kuwatamkia hivyo.

Hata hivyo alidai wapo ambao walidhani anatania kwani kasumba iliyopo huko ni kwamba vijana wengi wa mjini tabia zao si za kuoa kijijini kwani wanapenda sana wanawake waliyojipondoa na wale wanaovaa nguo fupi zinazoacha mwili nje.

“Ni kweli nilisafiri kama unavyojua mzazi ukiwa hujamuona siku kibao lazima ukamtembelee na kuzungumza naye lakini kikubwa nilichokifanya kwanza ni kutangaza kuwa nataka kuvuta jiko awali walizani nafanya utani, na niliamua hivyo kwa sababu kuna mtoto nilikuwa nampenda kitambo sana hivyo huyo anaweza kuwa mke wangu endapo kila kitu kitaenda sawa,” alisema.
TUPE MAONI YAKO
 

SULEIMAN MAGOMA Copyright © 2011 -- Template created by Suleiman Magoma -- Powered by Magoma Co.LTD