Rapper wa kike toka YMCMB Nicki Minaj hivi karibuni
ameelezea jinsi alivyobadilishwa kinidhamu na shandano la kutafuta vipaji vya
kuimba nchini Marekani ‘American Idol’ na kwamba amekuwa committed na shindano
hilo tofauti kabisa na hapo mwanzo.
The Hip Hop Queen wa Young Money ambae ni jaji wa mashindano
hayo amesema amejifunza kwenda na muda na kumeet deadline, na jopo la majaji
wenzake limemfanya awe na discipline.
“Waliponitajia , kama mwaka jana, nilidhani walikuwa
wanatania, producer Nigel alikuja kwangu na kusema, ‘tunataka kuongea na wewe
uwe jaji...’ walichukua muda mrefu, kiukweli sijazoea kutokea sehemu nayotakiwa
kuwa kwa muda muafaka. Nimekuwa my own boss kwa miaka michache, kwa hiyo hii ni
kama imeniongezea discipline kwenye maisha yangu. Hii imeongeza utawala
madhubuti kunibana nifanye kitu flani. Kila mtu aliathiriwa na nilichokuwa
ninafanya.” That’s Nicki Minaji.
‘The Freedom singer’ alionesha kuwa na tabia ya kuchelewa
kwenye matukio kama alivyokiri, na siku ya kwanza tu aliyokuwa anaungana na
majaji wenzake alichelewa kuingia kwenye mashindano hayo na alionesha hili
kwenye reality show yake ‘My Truth’ ambapo alionekana akihaha kujitahidi
asichelewe kuingia kwenye show hiyo coz sasa alikuwa anafanya kazi ya boss
mwingine na sio kuwa ‘her own boss’ kama alivyozoea.
Muda mfupi baada ya kuungana na majaji wa shindano hilo
Nicki alianzisha varangati kubwa na the R&B Diva Mariah Carey na akampiga
mkwara mbele ya majaji wenzake baada ya kutofautiana katika kutoa maamuzi na
comment zao kwa washiriki huku akimtuhumu Mariah kwa kumkatiza na kuingilia
alichokuwa anaongea.
Akiongea kuhusu Mariah kwenye reality show yeke ‘My
Truth’Nicki alisema “Nadhani Mariah amekutana na size yake kipindi hiki, na
sidhani kama alikuwa anatarajia kukutana na size yake kipindi hiki, am super
nervous, and anxious for the first day on ‘American Idol’....!”
Hayo ni baadhi ya maneno aliyosema Nicki Minaj behind the
scene ya American Idol, lakini sasa anakiri kuwa amefunzwa discipline na
mashindano hayo ikiwa ni pamoja na kufata muda uliopangwa kwa wakati.
Inawezekana pia imemfunza kuwa mvumilivu wakati anakutana na changamoto toka
kwa star mwenzake hasa ikiwa katika public, may be!!
